Credit Reference Bureaus (Swahili)
Kampuni ya Mogo Credit LTD ("Mogo") imepata leseni kutoka kwa Benki Kuu ya Tanzania kama Mtoa Huduma wa Mikopo Midogo asiepokea amana. Kama sehemu ya majukumu yetu ya kisheria, tunatakiwa kutoa taarifa za mkopo za mteja (zote chanya na hasi) kwa Makampuni ya Taarifa za Mikopo (CRB) yaliyosajiliwa.
Taarifa hizi zinaweza kutazamwa na Benki za Kibiashara, Taasisi za Mikopo, Vikundi vya Akiba na Mikopo (SACCOS), na watoaji wengine wa mikopo walio na leseni ili kukagua uwezo wako wa kukopa kwa maombi mapya au kwa madhumuni mengine yaliyoidhinishwa na sheria.
Athari kwenye Historia yako ya Mkopo (Credit Score)
- Ukilipa mkopo wako kulingana na makubaliano, historia hii nzuri ya malipo itashirikishwa na CRB na itakuwa na athari nzuri kwenye upatikaniji wako wa mikopo.
- Ikiwa akaunti yako itaingia kwenye makato, taarifa kuhusu malipo yaliyochelewa na idadi ya siku zilizopita zitashirikishwa. Hii itaathiri vibaya upatikanaji wako wa mkopo. Tafadhali kumbuka kuwa taarifa hii hasi itawailishwa tu ikiwa deni lako litakapofika muda wake na bado halijalipwa.
Taarifa kabla ya Kuwasilisha Taarifa hasi
Kabla ya kuripoti taarifa hasi za mkopo (kama vile kutokulipa), Mogo itakupatia notisi ya siku 30 ili urekebishe hali ya akaunti yako. Ikiwa makato hayatalipwa ndani ya muda huu wa notisi, Mogo ataendelea kuwasilisha data husika kwa CRB zilizo na leseni bila taarifa za ziada.
Ili kulinda historia yako ya mkopo, unashauriwa kulipia makato yoyote yaliyobaki na kuhakikisha kuwa makato yote ya baadaye ya mkopo yanalipwa kulingana na ratiba yako ya malipo.
|
Credit Info Limited Ghorofa ya 8 – Tanzanite Park |
Dun & Brad Street Credit Bureau Tanzania Ghorofa ya 12, PSPF Golden Jubilee Towers |
Haki yako ya Kupatia Taarifa yako ya Mkopo
Una haki ya kupata nakala ya ripoti yako ya mkopo. Unaweza kuomba ripoti hiyo moja kwa moja kutoka kwa CRB zilizo na leseni kwa anuani zifuatazo:
Kwa ufafanuzi wowote au maswali kuhusu mchakato huu, tafadhali wasiliana nasi kwa +255 690 000 222 au kupitia barua pepe kwa info@mogo.co.tz